Nenda kwa yaliyomo

Toby Alderwiereld

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Toby Alderwiereld

Toby Alderwiereld (matamshi ya Kiholanzi: [toːbi ɑldərβ̞ɛːrəlt]; kwa kirefu Tobias Albertine Maurits Alderweireld; alizaliwa 2 Machi 1989) ni mchezaji wa soka wa Ubelgiji ambaye anacheza Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Ubelgiji. Hasa ni mlinzi wa kati, anaweza pia kucheza kama beki wa pembeni.

Alderweireld alianza kazi yake ya kitaalam katika klabu ya Uholanzi Ajax, ambako alifanikiwa kushinda makombe matatu mfululizo ya Eredivisie.

Mwaka 2013, alihamia Atlético Madrid, ambapo alishinda La Liga na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa wa UEFA msimu wake wa kwanza.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Toby Alderwiereld kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.