Tin Hinan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tin Hinan

Mchoro wa mafuta unaomonyesha, Malkia Tin Hinan, uliochorwa na Hocine Ziani.
Nchi Algeria

Tin Hinan alikuwa malkia wa kabila la Watuareg katika karne ya 4. Kaburi kubwa linaloweza kuwa lake liko katika jangwa la Sahara, huko Abalessa, katika eneo la Hoggar, nchini Algeria.

Malkia wa Hoggar[hariri | hariri chanzo]

Hadithi za kale[hariri | hariri chanzo]

Tin Hinan mara nyingine huitwa Malkia wa Hoggar[1][2] na kwa Watuareg anaitwa Tamenokalt ambalo pia lina maana ya malkia.[3] Jina hilo lina maana ya mwanamke wa mahema,[3] lakini inaweza kutafsiriwa kwa mfano kama mama yetu sote.[4]

Kulingana na hadithi zilizosimuliwa katika eneo hilo, Tin Hinan alikuwa "malkia mkimbizi" ambaye aliishi wakati fulani katika karne ya 4 BK. Akiongozwa kutoka sehemu za kaskazini mwa Sahara, yeye na msafara wake wa wafuasi, kulingana na hadithi hizo, walikaribia kupotea jangwani hadi walipopata nafaka katika makaka ya jangwani. Katika hadithi nyingine ambazo hazijathibitishwa sana, Tin Hinan amewahi kutajwa kama Muislamu. Katika hadithi hii, Tin Hinan alikuwa na binti (au mjukuu), ambaye jina lake ni Kella, wakati Takamat alikuwa na mabinti wawili. Watoto hawa wanadaiwa kuwa mababu wa Tuareg wa Ahaggar. Toleo lingine linasema kwamba Tin Hinan alikuwa na mabinti watatu (ambao walikuwa na majina yanayohusiana na wanyama wa jangwani) ambao walikuwa mababu wa kikabila.

Kaburi la Tin Hinan[hariri | hariri chanzo]

Kufikia mwanzoni mwa karne ya 20, hadithi ya Tin Hinan ilikuwa imeelezewa kwa muda mrefu, na wengi waliamini kuwa ilikuwa tu hadithi au hadithi ya kufikirika. Hata hivyo, mwaka 1925, wapelelezi waligundua kaburi lake, wakithibitisha kwamba alikuwa mtu wa kweli katika historia. Lilipo siyo mbali kutoka katika kisima cha Abalessa, Algeria, takriban maili 1,000 (kilomita 1550) kusini mwa Aljeri, juu ya kilima kilichoinuka kama futi 125 (mita 38) juu ya mwingiliano wa mito miwili, Kaburi la Tin Hinan lina sura kama ya peari katika mpango wake na mhimili mkuu wa takriban futi 88 (mita 27). Linajumuisha vyumba 11 au viwanja.

Kaburi la Tin Hinan lilifunguliwa na Byron Khun de Prorok kwa msaada kutoka katika jeshi la Kifaransa mnamo mwaka 1925, na wanaakiolojia walifanya uchunguzi kamili zaidi mnamo mwaka 1933. Lilikutwa kuwa lina mifupa ya mwanamke (labda alizikwa katika karne ya nne BK) kwenye kigari cha kuni, akiwa amelala kifudifudi na kichwa chake kikiangalia upande wa mashariki. Alikuwa ameandamana na vito vya dhahabu na fedha nzito, baadhi yake ikiwa imepambwa na lulu. Mkono wake wa kulia alivaa bangili 7 za fedha, na kushoto, bangili 7 za dhahabu. Bangili nyingine ya fedha na pete ya dhahabu ziliwekwa pamoja na mwili. Mabaki ya mkufu wa kuvutia wa dhahabu na lulu (halisi na bandia) pia yalikuwepo.

Pia, vitu vya mazishi vilipatikana. Hivi ni pamoja na sanamu ya Venus, kikombe cha glasi (kimepotea wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia), mishale ya chuma yenye miiba, kisu cha chuma, na foil ya dhahabu ambayo ilibeba alama ya sarafu ya Kirumi ya Konstantino Mkuu iliyotolewa kati ya mwaka 308 na 324 BK. Tarehe ya karne ya 4 hadi ya 5 ni sawa na upimaji wa kaboni wa kitanda cha mbao na pia na mtindo wa vyombo vya udongo, kama vile taa ya udongo ya aina ya Kirumi ya karne ya tatu, na samani zingine za kaburi.Mijalada ya Tifinagh imeandikwa kwenye mawe ya ukuta. Kaburi lenyewe limejengwa kwa mtindo unaosambaa sana katika Sahara.

Utafiti wa anthropolojia ulihitimisha kuwa mifupa ilikuwa ya mwanamke Mnarabu mwenye umri wa wastani na mrefu. Sasa mwili uko katika Makumbusho ya Taifa ya Bardo huko Aljeri.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Huguenin-Gonon, N. (1973). Algeria. Nagel Publishers. uk. 137. ISBN 978-2-8263-0604-7. 
  2. Wellard, James (1965). The Great Sahara. London: Hutchinson & Company. uk. 47. 
  3. 3.0 3.1 "The World & I", Washington Times Corporation, 1987, p. 490. 
  4. Frawsen, Ulbani Ait; Ukerdis, L'Hocine (2003). "The Origins of Amazigh Women's Power in North Africa: An Historical Overview". Al-Raida (100): 19. 
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tin Hinan kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.