Thomas Menino

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Novemba 16, 1993 - Januari 6, 2014 [1]

Thomas Michael Menino (27 Desemba 1942 - 30 Oktoba 2014) alikuwa mwanasiasa wa Marekani ambaye aliwahi kuwa meya wa 53 wa Boston, kutoka 1993 hadi 2014. Alikuwa meya wa muda mrefu zaidi wa jiji hilo.

Alichaguliwa kuwa meya mwaka 1993 baada ya kutumikia nafasi ya "kaimu meya" kwa miezi mitatu. alichaguliwa kuwa meya baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake Raymond Flynn (aliyekuwa ameteuliwa kuwa balozi wa Marekani katika Ukulu mtakatifu). Kabla ya kutumikia kama meya, Menino alikuwa mjumbe wa Halmashauri ya Jiji la Boston na alichaguliwa kuwa rais wa Halmashauri ya Jiji hilo mnamo 1993.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Thomas Menino kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.