Nenda kwa yaliyomo

Tha Trademarc

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Marc Predka (anajulikana kwa jina la kisanii kama Tha Trademarc; alizaliwa 21 Aprili 1975) ni mwanamuziki wa Rap kutoka Marekani.

Mara ya kwanza kujulikana kwa umaarufu ilikuwa wakati yeye na binamu yake wa kwanza mwanamiereka wa WWE John Cena walishirikiana mnamo 2005 kutoa albamu You Can't See Me. Pia anaonekana katika video za nyimbo , ‘’Bad Bad Man’’ na ‘’Right Now’’ ambazo amefanya na John Cena. Leo hii yeye hufanya kazi katika kitengo cha elimu ya waiosjiweza katika Shule ya Maynard kule Maynard, Massachusetts.

Mnamo Agosti 2007, Trademarc alionekana katika miereka ya Total Nonstop Action Wrestling, ‘’Hard Justice’’ kama ‘’Mpenzi mpya’’ wa Karen Angle, ambayo baadaye ilithibitishwa kuwa uvumi wakati Karen na Trademarc walimsaidia bwanake Kurt Angle kushinda mechi[1].

Alionekana tena katika iMPACT! wiki iliyofuatia .[2]. Akiendelea kufanya kazi na TNA, alitoa wimbo wa kiingilio wa Kurt Angle ‘’Gold Medal’’ ambao aliufanya kwa kuchanganya rap kutoka Lunatic Fringe na utunzi wa TNA wa "My Quest". Mnamo 2008 alitoa solo Albamu yake ya kwanza Inferiority Complex.

East Coast Avengers

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Aagosti 2008 Trademarc aliungana na wasanii wa rap kutoka Massachusetts Esoteric na DC The Mid Alien kuunda kundi la East Coast Avengers. Albamu yao ya kwanza ilitoka baadaye 2008 ikiitwa Prison Planet. Kufikia sasa wametoa single iliyo na utata ya "Kill Bill O'Reilly" wakionyesha kuudhika kwao kwa msimulizi wa maswala ya siasa Bill O'Reilly na show yake katika televisheni ya Fox News Channel [3]. Katika wimbo huu wanaongelea jinsi O’Reilly huongea uongo na kubadili ukweli mara kwa mara. Uchambuzi wa wimbo huo na Michelle Malkin uliwafanya kutoa wimbo mwingine wa "Dear Michelle" kama jibu. .[4]. Wametoa pia wimbo mwingine uitwao "Hey America".

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Akimshirikisha John Cena

[hariri | hariri chanzo]

Peke yake

[hariri | hariri chanzo]

Akiwashirikisha East Coast Avengers

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Hard Justice 2007 results". Online World of Wrestling. Iliwekwa mnamo 2007-09-06.
  2. "TNA iMPACT! results - August 16, 2007". Online World of Wrestling. Iliwekwa mnamo 2007-09-06.
  3. Wells, Steven (2008) "Rap group call for the death of Bill O'Reilly", The Guardian, 19 Agosti 2008
  4. Crawford, Byron (2008) "No, really, kill Bill O’Reilly Archived 13 Septemba 2008 at the Wayback Machine.", XXLmag, 22 Agosti 2008

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tha Trademarc kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.