Nenda kwa yaliyomo

Mtete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tete (mmea))
Mtete
(Phragmites australis)
Mitete
Mitete
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama jaja)
Oda: Poales (Mimea kama manyasi)
Familia: Poaceae (Mimea iliyo mnasaba na manyasi)
Nusufamilia: Arundinoideae
Jenasi: Phragmites
Adans.
Spishi: P. australis
(Cav.) Trin. ex Steud.

Mtete au gugumua (Phragmites australis) ni aina ya nyasi refu linalomea katika maji kame. Jina hili hutumika pia kwa manyasi marefu yoyote ya maji. Aina za mimea ya maji zinazofanana na mtete huitwa mifunjo (familia Cyperaceae). Jenasi Phragmites inafikiriwa na bingwa wengi ya kuwa na spishi moja tu, lakini spishi nyingi zimefafanuliwa. Spishi moja, P. karka, husadikiwa sana.

Jina matete hutumika pia kwa manyasi haya, lakini inapendelewa kutumia jina hili kwa mazao yao. Matete hutumika duniani kote kwa kuvimba mapaa.