Teknolojia ya Akamai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Teknolojia ya akamai

Akamai Technologies ni kampuni ya Marekani inayojihusisha na utoaji huduma ya mtandao hivi kwamba unapotembelea wavuti fulani, waweza kufikia faili unazotaka kwa urahisi zaidi kana kwamba seva ya wavuti hiyo iko karibu na ulipo. Teknolojia hii huitwa content delivery network (CDN). Kampuni hii ina makao makuu huko Cambridge, Mashachuttes, Marekani.

Akamai Technologies ni miongoni mwa kampuni kubwa zaidi ulimwenguni kwa kupeana huduma ya mtandao kwa kutumia program ya Akamai netsession client interface iliyoko kwa tarakilishi ya mteja. Hii kampuni imehusishwa na asilimia kati ya 15 hadi 30 ya data ipatikanayo kwa mtandao.

Mbali na hayo, Akamai Technologies ina seva kwote ulimwenguni ambapo zinginezo zimekodishwa kwa wateja wanaotaka tovuti zao zifanye kazi haraka na kwa wepesi. Unapoingia katika tovuti ya Akamai Technologies, kivinjari chako kitabadislihwa na utaelekezwa kwa moja kati ya tovuti ya hii kampuni

Akamai Technologies ilianzishwa mnamo mwaka wa 1998 na Daniel M. Lewin wakiwa pamoja na Tom Lieghton ingawapo Tom Leighton aliuawa katika shambulizi lililotukia mnamo Septemba 11 mwaka wa 2001.Leighton kwa wakati huu ndiye Mkurugenzi Mtendaji. Akamai ni jina la kihawaiii linalomaanisha ‘ujanja’ kwa maana teknolojia yao ina ujanja wa kuwasilisha wavuti kwako kwa haraka.

Historia ya Akamai Technologies[hariri | hariri chanzo]

Kampuni ya Atakamai Technologies illingia katika mashindano na MIT iliyohusisha kuwashilisha fikra za kibiashara ambapo Akamai Technologies iliibuka kama moja ya kampuni zilizochaguliwa kwenda finali. Mnamo Agosti 1998, kampuni hii illikua imetengeneza prototaipu ya kibiashara.Hii ilikua kutokana na usaidizi wa Randall Kaplan,Jonathan Seelig, na Preetish Nijhawan. Mwaka wa 1998 ukielekea kumalizika, wataalamu wapya waliongezewa kujiunga na timu hii. Wanaojulikana sana ni Paul Segan aliyekua Rais wa Kampuni ya New Media, George Conrades aliyekua mwenyekiti wa kampuni ya BBN. Mnamo mwaka 1999, Conrades aliteuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji ambapo aliiongoza hii kampuni mpaka ikanoga kibiashara. Mnamo mwaka 2005 alimteua mwenzake Sogan kuwa mkurugenzi mtendaji. Mnamo Aprili 1999, Akamai Technologies iliidhinisha huduma ya kibiashara na ikatajwa kwa mara ya kwanza katika soko la hisa la NASDAQ.

Mnamo 1 Julai 2001, Akamai Technologies iliongezwa kwa sajala ya Russel 3000 na sajala ya Russel 2000. Mwakani 2001, mmoja wa waanzilishi wa kampuni,Daniel M. Lewin aliaga kutokana na tukio la ushambulizi wa ndege. Aliaga akiwa na miaka 31.Lewin alikua mmoja wa abiria waliokuwemo kwa ndege iliyoigonga jengo la World Trade Center. Mwakani 2005, Paul Segani aliteuliwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Akamai Technologies.Sagan alihakikisha kwamba kampuni hii imejitenga na wapinzani kwa lolote lile na kuwa mbele zaidi. Alifanya hivi kwa kuongeza huduma ambazo kampuni hii ilikua ikipeana. Kwa sababu ya uongozi wake na uadilifu,Akamai Technologies ilijikuza hadi kiwango cha mapato bilioni 1.37.Sagan aliiongoza Akamai Technologies kama mkurugenzi mtendaji hadi mwakani 2013 ambapo mkurugenzi mtendaji wa sasa,Tom Leighton alipoteuliwa.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Teknolojia ya Akamai kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.