Nenda kwa yaliyomo

Taribo West

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Taribo West (alizaliwa Port Harcourt, 26 Machi 1974) ni mchungaji na mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu wa Nigeria, aliyecheza kama beki.

Historia ya Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Taribo West alianzia maisha ya soka katika Vilabu vya mtaani kabisa (Obanta United) nchini Nigeria. Monday Sinclair ndiye mtu aliyegundua kipaji cha Taribo west na kumpeleka kwenye klabu ya Sharks ambayo iko rivers state mwaka 1990 na hakudumu Sana sharks fc akajiunga na Enugu Rangers na Julius Berger 1992. Hapa kipaji chake kilionekana na hatimaye akapata nafasi ya kujiunga na klabu ya Auxerre Ya Ufaransa, alicheza kwa kiwango kikubwa na Bora sana Katika klabu hii na akaweza kusajiliwa kwani Alienda kufanya Trial mwaka 1993 na mwaka 1997 akasajiliwa na Inter Milan, alifanikiwa kucheza Vilabu vingi vikubwa ikiwemo Ac Milan na pia Derby Country, Partizan, FC Kaiserslautern, Al Arab, Ply Mouth na Paykan

Maisha ya ndoa ndiyo yaliyompotezea kiwango chake uwanjani, baada ya kuachana na mkewe Mnigeria mwenzie Atinuke Ekundayo alifilisika baada ya talaka iliyomtaka amlipe mkewe mamiliioni ya pesa alishuka kiwango stress nyingi akaachana na soka.

Mwaka 2014 Taribo West aliamua kuanza kumtumikia Mungu na sasa ni miongoni mwa Wachungaji maarufu akihubiri Injili na kuelezea kufanya miujiza. Taribo West ni mwanzilishi wa Kanisa la Shelter In The Storm Miracle Ministries of All Nation la nchini kwao.

Enzi zake alijizolea umaarufu mkubwa kwa mtindo wake wa uchezaji ikiwemo 'mikogo' timu yake inapokuwa mbele pamoja na mitindo mbalimbali ya nywele.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Taribo West kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.