Sylvia Bahame

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sylvia Bahame (alizaliwa 20 Juni 1983) alikuwa Mrembo wa Tanzania kwa mwaka wa 2003.

Sylvia alianza elimu ya msingi mkoani Arusha, baadae akaenda kumalizia nchini Saudia, Oman, kisha kujiunga na elimu ya sekondari akiwa hukohuko Saudia na kumaliza mwaka 2001.

Kazi na Masomo[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2001 alirudi nchini Tanzania na familia yake ambapo alifanya kazi ya kufundisha katika shule moja hivi ya jijini Dar es Salaam maarufu kama Dar es Salam Independent ambapo alikuwa akifundisha darasa la pili na la tatu.

Mwaka wa 2002 akajiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisomea masomo ya sheria. Mpaka anakuwa Mrembo wa Tanzania alikuwa ana mwaka wa pili toka aanze kusoma Chuo Kikuu.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sylvia Bahame kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.