Susan Mashibe
| Susan mashibe | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Kazi yake | uhandisi na urubani wa ndege |
Susan Mashibe (alizaliwa 1973) ni mkurugenzi na muasisi wa kampuni ya Tanjet, kampuni ya kimataifa na ya kwanza ya aina yake nchini Tanzania inayoshughulikia masuala ya kiufundi katika ndege binafsi, za biashara na hata za diplomasia[1].
Maisha yake
[hariri | hariri chanzo]Alipokuwa na umri wa miaka minne alitamani kuendesha ndege, na baadaye katika umri wa miaka 19 yeye alitoka nchini Tanzania akaenda kusoma marekani katika chuo cha Western Michigan.
Alipomaliza masomo yake alitunukiwa cheti cha FAA cha uhandisi na urubani wa ndege.[2] Ndiye mwanamke wa kwanza nchini Tanzania kutambulika na FAA kama mhandisi na rubani wa ndege.
Baada ya tukio la mfuatano wa mashambulizi manne yaliyotekelezwa na kundi la kigaidi la Al-Qaeda nchini Marekani mnamo 11 Septemba 2001, Susan aliamua kurudi Tanzania; baadaye mwaka 2003 alianzisha kampuni iitwayo Tanjet ambayo kwa sasa inaitwa VIA.[3]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhia". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-12-22. Iliwekwa mnamo 2018-09-12.
- ↑ https://www.weforum.org/people/susan-mashibe
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-18. Iliwekwa mnamo 2018-10-17.
| Makala hii kuhusu wasifu wa Mtanzania bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |