Sululu-uzuri
Mandhari
(Elekezwa kutoka Sururu-uzuri)
Sululu-uzuri | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Sululu-uzuri (au Sururu-uzuri) ni ndege wa jenasi Rostratula na Nycticryptes katika familia Rostratulidae. Wakifanana na sululu, kwa kweli wana mnasaba zaidi na sile-maua. Wana rangi kali kuliko sululu na jike, kama yule wa sile-maua, ni mkubwa na ana rangi kali zaidi kuliko dume ambaye huatamia mayai na kutunza makinda. Wanatokea katika vinamasi na mabwawa ya matete na hutembea wakati wa utusitusi na mwanzo wa usiku. Hula mbegu, wadudu, gegereka, makoa na nyungunyungu. Jike hutaga mayai 2-4 ndani ya tundu juu ya biwi la mimea.
Spishi ya Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Rostratula benghalensis, Sululu-uzuri Mkubwa (Greater Painted Snipe)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Nycticryptes semicollaris (Lesser Painted Snipe)
- Rostratula australis (Australian Painted Snipe)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Sululu-uzuri mkubwa
-
Australian painted snipe