Sile-maua ni ndege wa familia ya Jacanidae. Ndege hawa wana vidole virefu ili kutembea juu ya majani ya myungiyungi na majani mengine yanayoelea. Wana kigao kidogo juu ya domo, isipokuwa sile-maua mdogo. Manyoya ya jinsia ni sawa, lakini jike anaweza kuwa mkubwa kidogo kuliko dume na kuanzisha ubembelezi; yule wa spishi nyingine (hususa Jacana spinosa) hukanyagwa na madume kadhaa. Dume huatamia na kutunza makinda. Sile-maua hula wadudu kwa majani na juu ya maji.