Sile-maua
Mandhari
(Elekezwa kutoka Microparra)
Sile-maua | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Sile-maua ni ndege wa familia ya Jacanidae. Ndege hawa wana vidole virefu ili kutembea juu ya majani ya myungiyungi na majani mengine yanayoelea. Wana kigao kidogo juu ya domo, isipokuwa sile-maua mdogo. Manyoya ya jinsia ni sawa, lakini jike anaweza kuwa mkubwa kidogo kuliko dume na kuanzisha ubembelezi; yule wa spishi nyingine (hususa Jacana spinosa) hukanyagwa na madume kadhaa. Dume huatamia na kutunza makinda. Sile-maua hula wadudu kwa majani na juu ya maji.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Actophilornis africana, Sile-maua wa Afrika (African Jacana)
- Actophilornis albinucha, Sile-maua wa Madagaska (Madagascar Jacana)
- Microparra capensis, Sile-maua Mdogo (Lesser Jacana)
Spishi za mabara mengine
[hariri | hariri chanzo]- Hydrophasianus chirurgus (Pheasant-tailed Jacana)
- Irediparra gallinacea (Comb-crested Jacana)
- Jacana jacana (Wattled Jacana)
- Jacana spinosa (Northern Jacana)
- Metopidius indicus (Bronze-winged Jacana)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Sile-maua wa Afrika
-
Pheasant-tailed jacana (nje ya majira ya kuzaa)
-
Comb-crested jacana
-
Wattled jacana
-
Bronze-winged jacana