Steven McKellar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Steven McKellar ni mwanamuziki kutoka nchini Afrika kusini. Anajulikana vizuri kama Mwimbaji, kiongozi na mwandishi wa nyimbo wa kikundi cha bendi cha muziki kiitwacho Civil Twilight. Aliwahi kuimba na kuucheza muziki wake wa "Nobody Can Save Me" akiwa na Linkin Park katika tamasha la kumbukumbu ya Chester Bennington huko Hollywood Bowl. Mnamo mwaka 2017, McKellar aliachia kazi yake mwenyewe ikiitwa Dayvid.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

McKellar alizaliwa Cape Town, Afrika kusini. Alivyokuwa katika kipindi chake cha utoto na kukua, baba yake alikuwa akituhumiwa na makosa mbalimbali ya kufungwa jela. Mama yake alikuwa akicheza piano,akiendeleza mapenzi yake ya muziki. Miongoni mwa waliomshawishi sana katika kipindi kile alikuwa ni Jeff Buckley, Oasis, na Blur[1]. Mnamo mwaka alianza kuimba muziki na kaka yake Andrew na rafiki yake wa utotoni Richard Wouters, hapo ndipo ulipo kuwa mwanzo wa kuundwa Civil Twilight.[2]

Maisha ya kazi[hariri | hariri chanzo]

McKellar alihamia mjini Los Angeles, California mwaka 2005, akijihusisha na kazi tofauti tofauti kabla ya kuahamia huko Nashville, Tennessee mwaka 2008.[3]Akiwa kama mwanachama wa kikundi cha Civil Twilight, alikuwa akipanda jukwaani na msanii Young the Giant, Florence + the Machine, Smashing Pumpkins, Jimmy Eat World, Silversun Pickups, na Monsters and Men.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.tntmagazine.com/leisure-entertainment/interviews/interview-south-africas-civil-twilight-frontman-steven-mckellar/
  2. "Civil Twilight: A musical journey from Cape Town to Nashville". www.cbsnews.com (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-04-26. 
  3. Dave Paulson. "Nashville rockers Civil Twilight hail from South Africa". The Tennessean (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2022-04-26.