Steph-Nora Okere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Steph-Nora Okere ni mwigizaji na mwandishi wa Nigeria ambaye alipewa Tuzo Maalum ya Utambuzi kwenye Tuzo za City People Entertainment Awards mnamo mwaka 2016[1]. Mnamo mwaka 2015 Okere alikua Makamu wa Rais wa Chama cha Waandishi wa Hati wa Nigeria (SWGN)[2].

Maisha ya awali na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Okere alizaliwa Owerri kwenye Jimbo la Imo mji mkuu wa eneo la kusini mashariki mwa Nigeria lililochukuliwa na watu wa Igbo wa Nigeria. Katika umri mdogo alihamia jimbo la Lagos kusini magharibi mwa Nigeria na kupata elimu yake ya msingi katika "Shule ya Msingi ya St Paul" iliyoko Ebute Metta ambapo alipata "Cheti cha Kuitimu Elimu Ya Awali".Okere alirudi katika jimbo lake la asili kupata elimu ya sekondari. Okere alipata "Cheti cha Shule ya Upili ya Afrika Magharibi" katika "Shule ya Sekondari ya Akwakuma" iliyoko Jimbo la Imo. Okere alipata shahada ya Sanaa ya ukumbi wa michezo kutoka Chuo Kikuu cha Obafemi Awolowo[3][4].


Kazi[hariri | hariri chanzo]

Okere kabla ya kuanza kwa tasnia ya sinema ya Nigeria inayojulikana kama Nollywood alikuwa mwigizaji wa jukwaa na alijitokeza mara ya kwanza katika Tasnia ya sinema ya Nigeria mnamo mwaka 1994 akiwa na umri wa miaka 21[5].


Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Okere alishinda Tuzo Maalum ya Utambuzi katika tuzo za City People Entertainment Awards mnamo mwaka 2016[6].


Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Okere amezungumza hadharani juu ya kumpenda mwenzake Jim Iyke[7][8]. Okere ingawa ni Mtu wa Igbo lakini anaweza kuzungumza lugha ya Kiyoruba kwa ufasaha.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Steph-Nora Okere kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.