St James Park
Mandhari
St. James' Park ni uwanja wa mpira wa miguu huko Newcastle upon Tyne nchini Uingereza. Ni uwanja wa nyumbani wa klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza Newcastle United F.C.
Uwanja huu una uwezo wa kuketisha watu 52,354, ni uwanja wa soka wa saba kwa ukubwa nchini Uingereza.
St. James' pamekuwa eneo la nyumbani la Newcastle United tangu mwaka 1892 na umetumika kwa soka tangu 1880. Katika historia yake yote, upanuzi wa uwanja huo umesababisha migogoro na wakazi wa mitaa na baraza la mitaa.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu St James Park kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |