Nenda kwa yaliyomo

Korobindo (Ploceidae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sporopipes)
Korobindo
Korobindo paji-madoa (Sporopipes frotalis
Korobindo paji-madoa (Sporopipes frotalis
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Ploceidae (Ndege walio na mnasaba na kwera)
Ngazi za chini

Jenasi 5, spishi 10:

Korobindo ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Ploceidae. Kuna ndege wengine ambao wanaitwa korobindo katika familia Passeridae. Spishi hizi zinatokea Afrika tu.

Ndege hawa wanafanana na shomoro lakini wana mwenendo kama kwera. Wana rangi ya kahawa au kijivu juu na nyeupe chini. Hula mbegu hasa na beri na wadudu pia.

Spishi hizi hulijenga tago lao ndani ya msongo wa manyasi na pengine vijitu pia ambao umebandikiwa tawi la mti. Korobindo mpendakundi hujenga jengo kubwa la manyasi linaloweza kuwa na nafasi kwa matago zaidi ya 100. Majengo haya yapo katika miti au juu ya nguzo zilizowekwa na watu kama vile nguzo za umeme. Jike huyataga mayai 3-5.