Nenda kwa yaliyomo

Spider-Man

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Spider-Man

Spider-Man ni jina la shujaa wa kubuni anayeonekana katika vitabu vya vibonzo vya Marekani vilivyochapishwa na Marvel Comics. Utambulisho wa kweli wa Spider-Man ni Peter Parker, mwanafunzi na mpiga picha kutoka Queens, New York City ambaye aliumwa na buibui ya mionzi wakati wa tukio la sayansi, kutoka wakati huo alipata nguvu mpya zinazofanana na uwezo sahihi wa buibui. Tangu 1977 ilianza mfululizo wa TV wa Spider-Man. Lakini tangu miaka ya 2000 kumekuwa na filamu zake nyingi tu zilizochezwa kama Spider-Man lakini maarufu zaidi iliyocheza na Tobey Maguire mwaka 2002, 2004 na 2007 ambazo kwa pamoja ziliitwa trlilojia ya Spider-Man chini ya uongozi wake "Sam Raimi". Baadaye zikaibuliwa tena na mwongozaji Marc Webb kwa ajili ya 2012, The Amazing Spider-Man na The Amazing Spider-Man 2 chini ya mwigizaji "Andrew Garfield" kabla kutemwa rasmi na kuibuliwa tena mwaka 2017 na Spider-Man: Homecoming ambamo ndani yake kacheza "Tom Holland" ambaye alionekana kwanza kwenye Captain America: Civil War 2016 kabla kuja rasmi kama Spider-Man mpya 2017 na 2018 Avengers: Infinity War na nyingine ambayo itatoka 2019.