Sona Tata Condé

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sona Tata Condé ni mwanamuziki wa Guinea anayetambulika kimataifa. Sona Tata ni mwanachama wa kabila la Mandinka. Sona Tata ni maarufu sana nchini Guinea, haswa katika mji mkuu wa Conakry. Sona Tata Condé alirekodi albamu[1] yake ya Simbo ambayo imepewa jina la mumewe, mwaka wa 2007.

Wimbo huo wenye jina, Simbo, ni wimbo wa mapenzi kwa mumewe na kama nyimbo zake nyingi, hauimbwa tu katika lugha yake ya asili ya Malinke, bali katika lugha nyingine zinazotumika katika mji mkuu wa Guinea, Conakry, zikiwemo lugha ya Fula, Susu, Kifaransa na Kiingereza. [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]