Somethin' for the People

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Somethin' for the People
Somethin' for the People
Taarifa za awali
Miaka ya kazi1990–2000
StudioCapitol Records
Warner Bros. Records
  • Curtis "Sauce" Wilson
  • Rochad "Cat Daddy" Holiday
  • Jeff "Fuzzy" Young (deceased)

Somethin' for the People lilikuwa kundi la muziki wa R&B kutoka mjini Oakland, California, ambao waligonga pini kadhaa nchini Marekani mwishoni mwa miaka ya 1990.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kundi lilianzishwa mnamo mwaka wa 1990 na Curtis "Sauce" Wilson na Jeff "Fuzzy" Young, wote wanatokea mjini Oakland, California, pamoja na mwenyeji wa Los Angeles Rochad "Cat Daddy" Holiday. Kundi lilirekodi demo kadhaa na kuzisambaza madukani huko mjini LA, na baadaye wakaingia mkataba na Capitol Records, ambao baadaye waliwawezesha kutoa albamu yao ya kwanza mnamo mwaka wa 1993. Wakiwa kama watunzi wa nyimbo, wametunga nyimbo kwa ajili ya Samuelle, En Vogue, Brandy, na U.N.V.[1] Walivyohamia Warner Bros. Records, walizitoa upya albamu zao za awali mnamo 1996. Albamu yao ya pili, This Time It's Personal, ilibamba vibaya mno huko nchini Marekani na Kanada, mauzo yalifika platinum kwa kibao cha "My Love Is the Shhh!",[2]ambacho kilishika nafasi ya #4 nchini Marekani na #7 nchini Kanada, na kundi lilifanya kazi zaidi kama watunzi wa nyimbo na midundo kimafanikio, kwa kwa kuwatungia ngoma Will Smith and Adina Howard.[1] LP ya tatu, Issues, ilifuata mnamo mwezi wa Julai 2000.

Kifo cha Jeff "Fuzzy" Young[hariri | hariri chanzo]

Mmoja wa wanachama wa kundi hili Jeff “Fuzzy” Young amekufa mnamo tarehe 4 Machi, 2011 kwa tatizo la mshtuko wa moyo.

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Jina Lebo US Top R&B/Hip-Hop Albums[3] US Billboard 200[3]
1993 Somethin' for the People Capitol Records
ilitolewa tena na Warner Bros. Records, 1996)
66
1997 This Time It's Personal Warner Bros. Records 33 154
2000 Issues 23 124

Single[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Jina Nafasi ya chati[4] Albamu
Billboard Hot 100 US Hot R&B/Hip-Hop Songs Canadian Singles Chart UK Singles Chart[5]
1995 "You Want This Party Started" 29 Somethin' for the People
1996 "Can You Feel Me" 91
"With You" 98 34
1997 "My Love Is the Shhh!" 4 2 7 64 This Time It's Personal
"Think of You"
1998 "All I Do" 47 15
2000 "Bitch With No Man" 39 Issues

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 [Somethin' for the People katika Allmusic Biography], Allmusic.com.
  2. "Best-Selling Records of 1997". Billboard (BPI Communications Inc.) 110 (5): 76. January 31, 1998. ISSN 0006-2510. Iliwekwa mnamo May 29, 2015.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. 3.0 3.1 [Somethin' for the People katika Allmusic Billboard], Allmusic.com
  4. [Somethin' for the People katika Allmusic Billboard Singles]. Allmusic.com.
  5. Roberts, David (2006). British Hit Singles & Albums (toleo la 19th). London: Guinness World Records Limited. uk. 514. ISBN 1-904994-10-5.