Sinema Zetu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sinema Zetu ni kituo cha matangazo kirushacho matangazo yake katika nchi za Afrika mashariki. Kituo hiki cha televisheni kipo chini ya usimamizi wa kampuni ya Azam Media Group. Kituo hiki cha televisheni kinafahamika kwa sababu ya kurusha filamu za Kitanzania. Pia kituo hiki huwa kinatoa tuzo mbalimbali za filamu.