Sikusare kusi
Mandhari
Sikusare kusi (ing. autumnal equinox) ni moja ya sikusare mbili za mwaka yaani siku ya usawa wa muda wa mchana na usiku katika maeneo mbali ya kanda ya ikweta.
Sikusare kusi ni sikusare ambako kipindi cha mchana mrefu umekwisha na kipindi cha nusu mwaka kinaanza ambako usiku ni mrefu kuliko mchana. Kupunguka kwa muda wa mchana kunasababisha kuongezeka kwa hewa baridi hivyo katika nchi zenye majira baridi mimea huanza kuopoteza majani na kuandaa usingizi.
Sikusare kusi inakadiriwa kuwa 23 Septemba.