Siku ya vijana Duniani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Siku ya Vijana Duniani Nchini Korea Kaskazini

Siku ya vijana duniani ni siku iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa. Lengo la hiyo siku ni kuhamasisha angalizo kwa namna fulani ya masuala ya kitamaduni na kisheria yanayowahusu vijana. IYD ya kwanza iliadhimishwa tarehe 12 Agosti 2000.

Asili[hariri | hariri chanzo]

IYD ilianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo 1999 na kupitishwa kwa Azimio 54/120. [1]

Siku ya vijana duniani inaadhimishwa kila mwaka tarehe 12 Agosti. Inaidhinishwa kama fursa kwa serikali na taasisi nyingine za kuweka mwangalizo masuala ya vijana ulimwenguni. Sherehe hizo huambatana na matamasha, warsha, hafla za kitamaduni, na mikutano inayohusisha maafisa wa serikali kitaifa, serikali za mitaa na mashirika ya vijana ambayo hufanyika ulimwenguni kote.

Kaulimbiu ya Siku ya Vijana mwaka 2014 ilikuwa Vijana na Afya ya Akili. Kwa mwaka 2015, ilikuwa Vijana na Ushiriki wa Jamii. Mada ya Siku ya Vijana ya Kimataifa ya 2016 ilikuwa "Agenda ya 2030: Kuondoa umaskini na kupata matumizi endelevu na uzalishaji." [2] Kwa mwaka wa 2017, mada ya IYD ilikuwa "Vijana kujenga amani". Mada ya IYD 2018 ilikuwa "Sehemu salama za Vijana". Kwa njia hii itaendelea ambayo inatambua michango ya vijana kuzuia mizozo, kusaidia ujumuishaji, haki ya kijamii, na kudumisha amani. Kwa mwaka wa 2019, mada ya IYD ilikuwa "Kubadilisha elimu" ili kufanya elimu ijumuishwe na kupatikana kwa vijana wote.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]