Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
Mandhari
Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ni kampeni ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake.[1] Kampeni hii hufanyika kuanzia tarehe 25 Novemba na kumalizika tarehe 10 Desemba ya kila mwaka kwa ajili ya kupinga ukatili na kutetea haki za wanawake.
Siku hiyo ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1991,siku hii inaongozwa na Kituo cha kimataifa cha Wanawake tarehe 10 ilichaguliwa rasmi kuwa siku ya kilele cha maadhimisho haya ikiambatana na siku ya haki za binadamu duniani.[2][1]
Tangu mwaka 1991, zaidi ya asasi 6,000 na zaidi ya nchi 187 hushiriki katika maadhimisho haya. [3]
Maadhimisho
[hariri | hariri chanzo]Siku hizi 16 za kupinga ukatili wa kijinsia huambatana na siku mbalimbali ambazo huadhimishwa ndani ya siku kumi na sita za mwezi Novemba na Desemba.
- Novemba 25 – Siku ya kupinga ukatili na unyanyasaji dhidi ya wanawake
- Novemba 29 – Siku ya kimataifa ya watetezi wa haki za wanawake
- Desemba 1 – Siku ya Ukimwi duniani
- Desemba 5 – Siku ya kujitolea duniani
- Desemba 10 – Siku ya Kimataifa ya haki za binadamu
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "16 days of activism". UN Women www.unwomen.org. Iliwekwa mnamo 6 Desemba 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "WHO | 16 Days of Activism Against Gender Violence". www.who.int. Iliwekwa mnamo 2017-03-08.
- ↑ "About". 16 Days Campaign (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-29. Iliwekwa mnamo 2019-10-29.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |