Sibongile Mlambo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sibongile Mlambo ni mwigizaji wa Zimbabwe anayefanya shughuli zake nchini Marekani. Anafahamika kwa kuwa mhusika mkuu katika filamu za mwendelezo za tovuti ya Netflix ambazo ni Lost in Space (filamu ya mwaka 2018), filamu ya mwendelezo ya the Starz historical adventure television, Black Sails , Honey 3: Dare to Dance na The Last Face.[1] Pia anafahamika kwa uhusika wake kama Tamora Monroe katika filamu ya mwendelezo ya Teen Wolf, Donna katika filamu ya mwendelezo ya Freeform, Melusi katika mchezo wa Ubisoft.

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Mlambo alizaliwa Zimbabwe na baba yake ni daktari. Mlambo ana dada ambaye pia ni mwigizaji. [2] Mlambo aliondoka Zimbabwe mwaka 2005 kuelekea nchini Marekani kwaajili ya masomo yake. Ameishi Texas, New York na Hispania. Mwaka 2011 Mlambo alikuwa akiishi Afrika ya kusini na kufanya kazi zake Cape Town na Johannesburg. [3] Mlambo later moved back to the United States, settling in Los Angeles.[4] Mlambo alisoma kifaransa na kihispania katika chuo kikuu cha Methodist.[2]

Kazi yake[hariri | hariri chanzo]

Mitindo[hariri | hariri chanzo]

Mlambo alikuwa mwana mitindo katika kampeni ya Nivea barani Afrika . Mwaka 2007 Mlambo alikuwa mshindi wa pili katika shindano la walimbwende wa zim-USA. [5]

Uigizaji[hariri | hariri chanzo]

Ameigiza kama mhusika mkuu katika filamu ya Black Sails, Honey 3: Dare to Dance na Footloose. [6] Pia alikuwa mhusika mkuu katika filamu ya The Last Face aliyeigiza kama Assatu na alikuwa dada yake Chadwick Boseman katika filamu ya Message From The King. [7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Zim Actress Sibongile Mlambo to be Lead Actress in Honey 3. Z Gossip. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-28. Iliwekwa mnamo 22 May 2017.
  2. 2.0 2.1 Scott, Sydney (27 March 2018). 5 Things To Know: Sibongile Mlambo Is Set To Make A Splash In Freeform's 'Siren'. Essence.
  3. 10 Questions For: Sibongile Mlambo. Cape Town Magazine. Iliwekwa mnamo 22 May 2017.
  4. Sibongile Mlambo – Actress, United States. Zimbassador. Jalada kutoka ya awali juu ya 2020-01-31. Iliwekwa mnamo 22 May 2017.
  5. Holly Wood actress relishes Zim honour. Daily News (18 September 2016). Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-05-29. Iliwekwa mnamo 22 May 2017.
  6. Sibongile Mlambo: Zimbabwean-Born Actress Starrs in ‘Honey 3’. Face2Face. Iliwekwa mnamo 22 May 2017.
  7. Another Hollywood role for Zim actress. Nehanda Radio (15 May 2015). Iliwekwa mnamo 22 May 2017.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sibongile Mlambo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.