Nenda kwa yaliyomo

Shinikizo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
A figure showing pressure exerted by particle collisions inside a closed container. The collisions that exert the pressure are highlighted in red.
Shinikizo kutoka migongano ya chembe ndani ya chombo kilichofungwa

Shinikizo (kwa Kiingereza "pressure"; ishara yake ni p au P. Matumizi ya P au p inategemea tasnia au taaluma. Mapendekezo ya IUPAC ya kuonyesha shinikizo ni herufi 'p' ndogo.[1] Hata hivyo, herufi P kubwa hutumika sana.) ni kani inayotumika kutoka juu moja kwa moja kwenye uso wa kitu kwenye eneo kani hiyo imesambaziwa[2]

Safu ya Zebaki.

Vipimo mbalimbali hutumika kuonyesha shinikizo. Baadhi yake hutokana na kipimo cha kani kugawanywa na kipimo cha eneo hilo; kipimo cha SI cha shinikizo, Pascal (Pa), kwa mfano, ni nyutoni moja kwa kila mita ya mraba (N/m2, au kilo·m-1·s-2). Jina la kipimo hiki liliongezewa mwaka 1971;[3] mbeleni, shinikizo katika SI ilionyeshwa kama nyutoni kwa kila mita ya mraba..

Shinikizo inaweza pia kuonyeshwa kama shinikizo la anga la kawaida; anga (atm) ni sawa na shinikizo hili, na torr hufafanuliwa kama 1760 ya hii.

Vipimo manometric kama vile sentimita ya maji, milimita ya zebaki, na inchi ya zebaki hutumika kueleza shinikizo kwa suala la urefu wa safu ya kiowevu fulani katika manometer.

Kihisabati:

ambapo:

ni shinikizo,
ni ukubwa wa kani ya kawaida,
ni eneo la uso juu ya kugusana.

Inapotumika

[hariri | hariri chanzo]
  1. McNaught, A. D. (2014). IUPAC. Compendium of Chemical Terminology, 2nd ed. (the "Gold Book"). 2.3.3. Oxford: Blackwell Scientific Publications. doi:10.1351/goldbook.P04819. ISBN 0-9678550-9-8.
  2. Giancoli, Douglas G. (2004). Physics: principles with applications. Upper Saddle River, N.J.: Pearson Education. ISBN 0-13-060620-0.
  3. "14th Conference of the International Bureau of Weights and Measures". Bipm.fr. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-06-30. Iliwekwa mnamo 2012-03-27.
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shinikizo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.