Nenda kwa yaliyomo

Paskali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Pascal)

Paskali (pia: Pascal; kifupi: Pa) ni kipimo cha SI kwa kanieneo au shinikizo.

Inataja kani au nguvu inayoathiri eneo fulani ikiwa ni sawa na nyutoni kwa mita 1 ya mraba.

Jina lake lilichaguliwa kwa heshima ya mwanafizikia na mwanahisabati Mfaransa Blaise Pascal.

Katika maisha ya kila siku tunasikia habari za paskali katika habari za hali ya hewa ambako kanieneo angahewa inatajwa kila siku kwa hektopaskali "hPa" yaani paskali 100.[1]

Kipimo kingine kinachotumiwa mara nyingi ni kilopaskali "kPa" = paskali 1,000 kwa mfano kwa ajili ya shinikizo ya tairi.[2].

Kanieneo angahewa kwenye uwiano wa bahari inalingana takriban na kilopaskali 100 au hektopaskali 1,000. Zamani hii iliitwa pia bar 1. Kiwango cha kanieneo angahewa kikamilifu ni bar 1.01325 = Pa 101 325 = kPa 101,325 = hPa 1 013,25.

  1. World Meteorological Organization: Manual on the Global Observing System – Volume I, Section 3.3.2.2: "The hectopascal (hPa), equal to 100 pascals (Pa), shall be the unit in which pressures are reported for meteorological purposes."
  2. ISO 5775: Bicycle tyres and rims