Bar (shinikizo)
Mandhari
Bar (alama bar), pamoja na sehemu zake za desibar (alama dbar) milibar (alama mbar, pia mb) ni vizio vya shinikizo. Si vipimo vya SI lakini hunatumiwa kandokando na kizio cha SI cha paskali, hasa kwa taarifa za hali ya hewa na pia kwa kupima hewa ndani ya matairi.
Ufafanuzi
[hariri | hariri chanzo]- bar 1 = 1000 mbar = paskali (Pa) 100,000
- desibar (dbar) 1 = bar 0.1 = Pa 10,000
- milibar (mbar) = bar 0.001 = Pa 100
Bar 1 inalingana takriban na shinikizo la hewa kwenye ufuko wa bahari au
bar 1.01325 = paskali (Pa) 101 325 = kilopaskali (kPa) 101,325 = hektopaskali (hPa) 1 013,25.
Paskali ni kipimo cha SI kinachofafanuliwa kuwa sawa na nyutoni 1 kwa mita 1 ya mraba.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Jina bar linatokana na Kigiriki βάρος (baros) kinachomaanisha uzito. Alama rasmi ni "bar"; zamani ilikuwa "b" pekee na hii bado inaonekana katika kifupi cha "mb" badala ya "mbar" kwa milibar.