Nenda kwa yaliyomo

Sheila Gordon

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sheila Gordon (Johannesburg, Afrika Kusini, 22 Januari 1927 - 10 Mei 2013) alikuwa mwandishi Mmarekani aliyezaliwa nchini Afrika Kusini. Aliandika vitabu mbalimbali miongoni mwa hivyo ni Waiting for the Rain, The Middle of Somewhere, na Unfinished Business (riwaya).

Waiting for the Rain ni hadithi inayozungumzia simulizi ya vijana wawili wa kiume waliozaliwa na kukulia katika eneo la mashamba nchini Afrika kusini wakati wa ubaguzi wa rangi mmoja akiwa ni mwenye rangi nyeusi na mwingine mweupe,urafiki wao unaingia doa pale wanapokuwa wakubwa walipoingia katika siasa, mmoja mweusi akitafuta haki ya usawa katika siasa na kijana mwingine mweupe akitaka hali ibaki kama ilivyokuwa mwanzo.

Sheila aliishi katika mji wa Cobble Hill, karibu na mji wa mdogo wa Brooklyn kwa muda wa miaka hamsini.

Sheila alifariki akiwa na umri wa miaka 86 na mume wake alifariki miezi mitatu baada ya kifo cha Sheila mnamo tarehe 8 Agosti

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sheila Gordon kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.