Seetha Coleman-Kammula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Seetha Coleman-Kammula ni mwanakemia wa Kihindi, mwanamazingira na mjasiriamali.zaidi ya miaka 25 alifanya kazi katika tasnia ya petrokemikali ikitengeneza plastiki, alianza kampuni ya ushauri wa mazingira mnamo mwaka 2005. Kampuni yake inazingatia ikolojia ya kiviwanda na tathmini ya mzunguko wa maisha ya bidhaa ili zitengenezwe katika michakato inayofahamu mazingira juu ya athari ya siku zijazo ya bidhaa taka.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Seetha Coleman-Kammula alihudhuria masomo yake ya shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Osmania cha Hyderabad, India. Aliendelea na masomo ya PhD katika kemia ya kikaboni kutoka Chuo Kikuu cha Auburn huko Auburn, Alabama na kisha akafanya utafiti wake wa kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Princeton. Alitunukiwa Ushirika wa NATO na kumaliza masomo ya ziada katika Chuo Kikuu cha Amsterdam. Mnamo mwaka 1978, aliajiriwa kama mtafiti katika Royal Dutch Shell huko Amsterdam ambapo alifanya kazi hadi mwaka 1988. Baada ya miaka kumi, [1]alihama na Shell hadi Uingereza ambako alifanya kazi kama meneja wa maendeleo ya biashara.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Dr. Seetha Coleman-Kammula", Detroit, Michigan: Plastics News, 11 February 2008.