Nenda kwa yaliyomo

Saratani ya endometriamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Endometrial cancer
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuOncology
ICD-10C54.1
ICD-9182.0
OMIM608089
DiseasesDB4252
MedlinePlus000910
eMedicinemed/674 radio/253
MeSHD016889

Saratani ya endometriamu ni saratani inayotokana na endometriamu ( utando wa uterasi au tumbo la uzazi).[1] Hii hutokana na ukuaji usio wa kawaida wa seli zenye uwezo wa kushambulia au kuenea katika sehemu zingine za mwili.[2] Ishara ya kwanza mara nyingi huwa hali ya kutokwa na damu ukeni isiyohusishwa na hedhi ya kila mwezi. Dalili zingine zinajumuisha maumivu wakati wa kukojoa, maumivu wakati wa ngono au maumivu ya pelvisi.[1] Saratani ya endometriamu hutokea mara nyingi baada ya ukomohedhi.[3]

Kisababishi na Utambuzi

[hariri | hariri chanzo]

Takriban asilimia 40 ya visa hivi vinahusishwa na unene wa kupindukia.[4] Saratani ya endometriamu inahusishwa na mfichuo zaidi wa estrojeni , shinikizo la juu la damu na kisukari.[1] Huku kumeza estrojeni pekee kukiongeza hatari ya saratani ya endometriamu, kumeza mchanganyiko wa estrojeni pamoja na projesteroni kama ilivyo katika nyingi ya vidonge vya kudhibiti uzazi hupunguza hatari hii.[1][4] Takriban asilimia mbili hadi tano ya visa hivi huhusishwa na jeni zinazorithiwa kutoka kwa wazazi.[4] Saratani ya endometriamu wakati mwingine huitwa "saratani ya uterasi", ingawaje aina hii huwa tofauti na aina zingine za saratani ya uterasi kama vile saratani ya seviksi, sakoma ya seviksi, na ugonjwa wa trofoblasti.[5] aina ya saratani ya endometriamu inayotokea mara nyingi zaidi ni endometrioidi kasinoma, ambayo husababisha zaidi ya asilimia 80 ya visa.[4] Saratani ya endometriamu hutambuliwa mara nyingi katika biopsi ya endometriamu au kwa kuchukua vielelezo wakati wa utaratibu unaojulikana kama upanukaji na usafishaji wa kizazi. Uchunguzi wa seviksi kwa kawaida hautoshi kuonyesha saratani ya endometriamu.[6] Uchunguzi wa mara kwa mara kwa walio katika hatari ya kawaida hauhitajiki.[7]

Matibabu na Prognisisi

[hariri | hariri chanzo]

Matibabu makuu ya saratani ya endometriamu ni histerektomi ya fumbatio (kuondoa uterasi kabisa kupitia upasuaji), pamoja na utoaji wa neli za fallopia na ovari katika pande zote unaoitwa salpingo-uuforektomi ya pande mbili. Katika visa vingi vya kiwango cha juu, tiba ya mionzi, kemotherapi au tiba ya homoni pia inaweza kupendekezwa. Ikiwa ugonjwa utatambuliwa katika awamu ya mapema, matokeo huwa bora,[6] na jumla ya kiasi cha miaka mitano ya kuishi nchini Marekani huwa zaidi ya asilimia 80.[8]

Epidemiolojia

[hariri | hariri chanzo]

Katika mwaka wa 2012, saratani ya endometriamu ilitokea kwa wanawake 320,000 na kusababisha vifo 76,000 .[4] Hii inaifanya saratani hii kuwa ya tatu kuu inayosababisha vifo kati ya saratani zinazowaathiri wanawake baada ya ya ovari na saratani ya seviksi. Saratani hii hutokea mara nyingi katika nchi zilizoendelea[4] na ni saratani inayotokea mara nyingi zaidi ya mfumo wa uzazi wa kike katika nchi zilizoendelea.[6] Kiasi cha saratani ya endometriamu kimeongezeka katika nchi kadhaa kati ya miaka ya 1980 na 2010.[4] Hii inaaminika kutokana na idadi inayoongezeka ya watu wazee na viwaango vya juu vya unene wa kupindukia.[9]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "General Information About Endometrial Cancer". National Cancer Institute. 22 Aprili 2014. Iliwekwa mnamo 3 Septemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Defining Cancer". National Cancer Institute. Iliwekwa mnamo 10 Juni 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Kong, A; Johnson, N; Kitchener, HC; Lawrie, TA (18 Aprili 2012). "Adjuvant radiotherapy for stage I endometrial cancer". The Cochrane database of systematic reviews. 4: CD003916. PMID 22513918.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 4.5 4.6 International Agency for Research on Cancer (2014). World Cancer Report 2014. World Health Organization. Chapter 5.12. ISBN 978-92-832-0429-9.
  5. "What You Need To Know: Endometrial Cancer". NCI. National Cancer Institute. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-08-08. Iliwekwa mnamo 6 Agosti 2014. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 6.2 "Endometrial Cancer Treatment (PDQ®)". National Cancer Institute. 23 Aprili 2014. Iliwekwa mnamo 3 Septemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Hoffman, BL; Schorge, JO; Schaffer, JI; Halvorson, LM; Bradshaw, KD; Cunningham, FG, whr. (2012). "Endometrial Cancer". Williams Gynecology (tol. la 2nd). McGraw-Hill. uk. 823. ISBN 978-0-07-171672-7. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-01-04. Iliwekwa mnamo 2015-08-17. {{cite book}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20140104204142/http://www.accessmedicine.com/content.aspx?aID= ignored (help)
  8. "SEER Stat Fact Sheets: Endometrial Cancer". National Cancer Institute. Iliwekwa mnamo 18 Juni 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. Hoffman, BL; Schorge, JO; Schaffer, JI; Halvorson, LM; Bradshaw, KD; Cunningham, FG, whr. (2012). "Endometrial Cancer". Williams Gynecology (tol. la 2nd). McGraw-Hill. uk. 817. ISBN 978-0-07-171672-7. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-01-04. Iliwekwa mnamo 2015-08-17. {{cite book}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help); Unknown parameter |https://web.archive.org/web/20140104204142/http://www.accessmedicine.com/content.aspx?aID= ignored (help)