Sarafu ya Bit

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Sarafu ya Bit (kwa Kiingereza: Bitcoin) ni mfumo wa malipo dijitali ambao unatumiwa na mamilioni ya watu bila msimamizi wa juu kama Benki Kuu ilivyo katika nchi mbalimbali. Sarafu hiyo huweza kutumika kwa kubadilishana na sarafu nyingine, bidhaa au huduma.

Sarafu ya Bit ilianzishwa na mtu asiyejulikana au kikundi cha watu chini ya jina la Satoshi Nakamoto na kutolewa kama programu huria mwaka 2009. Kuanzia Februari 2015, wafanyabiashara zaidi ya 100,000 wanakubali bitcoin kama malipo.

Kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Cambridge wa mwaka 2017, kuna watu kati ya milioni 2.9 hadi 5.8 wanaotumia malipo dijitali na wengi wao wanatumia sarafu ya bit.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.jbs.cam.ac.uk/fileadmin/user_upload/research/centres/alternative-finance/downloads/2017-global-cryptocurrency-benchmarking-study.pdf

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sarafu ya Bit kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.