Salim Ahmedy
Salim Ahmed | |
---|---|
Gabo—2018 | |
Amezaliwa | Salim Ahmed Issa Juni 6, 1983 Muheza, Tanga, Tanzania Muheza |
Jina lingine | Gabo Zigamba |
Kazi yake | Mwigizaji, mwigizaji wa sauti, mtunzi wa filamu, mwongozaji, mtayarishaji |
Miaka ya kazi | 2008- |
Ndoa | Latifa Babla Ivan (Tiffany Stores) (2020) |
Watoto | 4 |
Salim Ahmedy Issa (amezaliwa Muheza, Tanga, 6 Juni 1983) ni mwigizaji, mwongozaji, mwandishi na mtayarishaji wa filamu kutoka nchini Tanzania.[1] Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Gabo Zigamba. Salim amekuwa akisifika kwa umahiri wake katika kuzishika nyusika tofauti. Anafahamika zaidi kwa kucheza filamu ya Big Surprise, Danija, Siyabonga, na nyingine nyingi. Pia ameonekana katika mifululizo ya runinga maarufu kama vile Jua Kali, Kapuni na Baba Olivia.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Salim alianza elimu ya msingi mnamo 1992 hadi 1998 katika shule ya Iringa Wilolesi. Baadaye sekondari katika shule ya Al-Haramain. Akamaliza 2002. Kuanzia 2003-2006 alijiunga na Chuo Darul Ulumi, Elimu ya Thanawiy. 2006 Chuo Cha Tasuba, Kozi ya Mwaka Mmoja upande wa sanaa. 2007 alijiunga na kampuni ya Super Loaf. Ambapo alifanyakazi mwaka mmoja pekee. Hapo alijikita zaidi kama mhasibu na baadaye akawa mchanganya viambata vya bidhaa.
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mwigizaji, umarufu
[hariri | hariri chanzo]Akiwa katika mahojiano ya kipindi cha Salama Na kinachotupwa mkondoni huko YouTube chini ya Salama Jabir , Salim alitoa siri ya chimbuko la jina la Gabo, "Asili ya jina ni Gabo ni Gabon. Lina maana ya 'sauti isiyosikika" na Zigamba, ni ng'ombe wa kimila aliyekuwa akiabudiwa na Wasukuma zama za kale. Kimsingi, Salim alianza uigizaji rasmi mnamo mwaka wa 2006. Akiwa katika kipindi cha awali kabisa kupoteana na ujalunga, yaani, umri wa miaka 23. Wakati huo alikuwa akisoma Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA). Kabla ya kufika kilele cha kufahamika, alijitupa katika makundi kadhaa ya uigizaji yaliyokuwa jijini Dar es Salaam huku ari ya kutaka kuwa mwigizaji nyota ikifika pomoni. Katika kutimiza ile ndoto ya miaka mingi, hatimaye akawemo katika filamu ya "Olopong" iliyotayarishwa na Al Riyamy Production iliyoongozwa na Khalfan Abdalah, ikafuatiwa na 007 Days.
Atafutaye hachoki, hata akichoka, basi keshapata. Dumu la kutojulikana lilipasuka rasmi mnamo mwaka 2012 baada ya kucheza katika filamu ya "Bado Natafuta." Yaliyomo ndani yake yakaonekana vema. Filamu hiyo alicheza na Patcho Mwamba, Zuberi Mohamed na Shamsa Ford.
Baada ya kufanya kazi, hatmaye akaanzisha kampuni yake ya utayarishaji wa filamu. Akaipa jina la Gabz Media Production (T) Limited.
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]Filamu
[hariri | hariri chanzo]Baadhi ya filamu za Gabo;
Na. | Jina la filamu | Mwaka | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|---|
1 | Bado Natafuta | 2012 | Mr. James | Mwongozaji Sulesh Marwa, Mtayarishaji Jerumasalem Films |
2 | Jicho Langu | 2014 | James | Mwongozaji: Leah Mwendamseke
Mtayarishaji: J-Film For Life Production |
3 | Kona | 2015 | Mjomba wa Zazuba | Mwongozaji: Salim Ahmedy[2]
Utayarishaji: Landline Production |
4 | Big Surprise | 2014 | Gabo | Mwongozaji: Leah Mwendamseke
Mtayarishaji: J-Film for Life Production |
5 | Danija | 2014 | Johnson | Mwongozaji: Jacob Steven (JB)
Mtayarishaji: Jerusalem Film Company |
6 | Safari ya Gwalu | 2015 | Gwalu | Mwongozaji: Daniel Manege
Mtayarishaji: Manege Entertainment |
7 | Kasanga Nae Mwana | 2016 | Zigamba | Utayarishaji: King Media |
8 | Heaven Sent | 2017 | Gabo | Mwongozaji: Neema Ndepanya
Mtayarishaji: Endless Fame Production |
9 | Siyabonga | 2017 | Siyabonga | Mwongozaji: Salum Majagi
Mtayarishaji: Sarafu Media |
10 | Dr. Okosovo | 2018 | Dr. Okosovo Kalababash | Mwongozaji : Salim Ahmedy
Mtayarishaji: Above The Rim Production |
11 | Sumu | 2018 | Salim | Mwongozaji: Patrick Komba
Mwongozaji Msaidizi: Salim Ahmedy Mtayarishaji: Third Eye Africa |
12 | Segere | 2019 | Chief Segere | Mwongozaji: Takura Maurai.
Mtayarishaji: Sarafu Media |
13 | Kesho | 2020 | Matete Mkandara | Mwongozaji: Salum Majagi
Mtayarishaji : Yusuph Mlela |
14 | Kigoma | 2020 | Gabo | Mtayarishaji: Mpakasi Films Company |
15 | Tug of War | 2021 | Koplo Matata | Mwongozaji: Amil Shivji
Mtayarishaji: Kijiweni Film Production |
Mifululizo ya Runinga
[hariri | hariri chanzo]Na | Jina la filamu | Mwaka | Jina la uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|---|
1 | Kapuni | 2019 | Mr. Brown | DSTV |
2 | Baba Olivia | 2020 | Baba Olivia | Pendwa App |
3 | Jua Kali | -2023 | Diba | DSTV |
4 | Bondeni | 2015 | ? | TBC1 pia ni mtayarishaji |
5 | Family Love | 2017 | ? | Clouds TV. Pia ni mtayarishaji |
6 | Maskani | 2021 | ? | Gabz Media |
Tuzo na Teuzi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Tamasha | Tuzo | Mshindi | Matokeo |
---|---|---|---|---|
2016 | Tuzo za ZIFF | Mwigizaji Bora | Salim Ahmedy | Ameshinda[3] |
2017 | Tuzo za EATV | Mwigizaji Bora | ? | Ameshinda[4] |
Tuzo za ZIFF | Mwigizaji Bora | ? | Ameshinda[5] | |
2018 | Tuzo za EATV[6] | Mwigizaji Bora | Ameshinda[7] | |
2018 | Tuzo za SIZIFF | Mwigizaji Bora | Ameshinda[8] | |
2021 | Tanzania Film Festival | Mswada Bora wa Filamu | Ameshinda[9] |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Exclusive interview na Gabo; Je ni teja,mmakonde au mchaga?". Bongo Publisher. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-07-22. Iliwekwa mnamo 2023-07-22.
- ↑ "Full Interview: Gabo Zigamba Akizungumzia Filamu Yake ya Kona 3". Artists News in Tanzania. 2016-02-28. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-07-22. Iliwekwa mnamo 2023-07-22.
- ↑ Ziff Awards 2016
- ↑ Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs namedeatv awards
- ↑ ZIFF Awards 2018
- ↑ "WAMBURA BABU BLOG: Ridhiwani afunguka ushindi wa Gabo EATV AWARDS". WAMBURA BABU BLOG. 2016-12-12. Iliwekwa mnamo 2023-07-22.
- ↑ Tuzo za EATV
- ↑ SIZIFF 2018
- ↑ Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>
tag; no text was provided for refs namedTZFF 2021
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Salim Ahmedy katika Instagram