Sakramenti za kuingizwa katika Ukristo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Sakramenti za Wakatoliki na Waorthodoksi

Kanisa Katoliki na yale ya Waorthodoksi na ya Waorthodoksi wa Mashariki yanaamini kwamba mtu anaingizwa katika Ukristo kwa sakramenti tatu zinazofungamana: ubatizo, kipaimara na ekaristi. Kabla hajazipokea zote tatu, mtu hahesabiwi kuwa Mkristo kamili.

Upande wa magharibi, maadhimisho ya sakramenti hizo yamefanyika mara nyingi kwa nyakati tofauti, na katika Uprotestanti kwa kawaida kipaimara hakitazamwi kuwa sakramenti iliyowekwa na Yesu Kristo, ila ibada au maombezi tu.