Sabina Wanjiru Chege
Jinsia | mwanamke |
---|---|
Nchi ya uraia | Kenya |
Jina halisi | Sabina |
Tarehe ya kuzaliwa | 10 Agosti 1978 |
Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihi | Kiingereza, Kikikuyu, Kiswahili |
Kazi | politician |
Nafasi ilioshikiliwa | Member of the National Assembly, Member of the National Assembly |
Alisoma | Chuo Kikuu cha Nairobi |
Honorific prefix | The Honourable |
Mwanachama wa chama cha siasa | National Alliance Party of Kenya |
Kabila | Wagikuyu |
Described at URL | http://www.parliament.go.ke/the-national-assembly/members/item/3950-hon-chege-maitu-sabina-wanjiru |
Sabina Wanjiru Chege (amezaliwa 22 Agosti 1978) ni mwanasiasa, muigizaji na mtangazaji wa zamani wa radio na runinga kutoka Kenya. Mwaka 2013 hadi 2022 alihudumu kama mbunge wa kaunti ya Murang'a.
Wasifu wa kisiasa
[hariri | hariri chanzo]Alichaguliwa kuwa mwakilishi wa wanawake katika Bunge la Kitaifa katika Kaunti ya Muranga mwaka wa 2013 kwa asilimia 96.6% ya kura. Alikuwa mwanachama wa chama cha National Alliance. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017, alichaguliwa tena, akiwa mwanachama wa Jubilee Party. Chama cha Jubilee kilianzishwa mnamo mwaka 2016 kama mrithi wa Jubilee Alliance, muungano wa vyama kadhaa vya kisiasa ikiwa ni pamoja na chama cha Chege cha National Alliance. Katika kipindi chake cha kwanza bungeni alikuwa mwenyekiti wa Kamati ya Idara ya Elimu, Utafiti na Teknolojia na mwanachama wa Kamati ya Usimamizi wa Utekelezaji wa Katiba. Tangu mnamo mwaka 2017 amekuwa akihudumu kama mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kwenye taasisi ya Afya.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Munuhe. "Inside story of why the Teachers Service Commission list was rejected", The Standard. (en)
Makala hii kuhusu mwanasiasa huyo wa Kenya bado ni mbegu. Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |