Roger Dubuis (mtu)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Roger Dubuis (alizaliwa Corbeyrier, kantuni ya Vaud, Uswisi, 1938 - 14 Oktoba 2017) ni mmmoja wa waanzilishi wa kampuni ya utengenezaji wa saa ya Roger Dubuis.

Alianza fani ya utengenezaji wa saa huko Longines katika miaka ya 1950 na baadaye alihamia kwenye karakana za Patek Phillippe ambako alikaa kwa miaka 14.

Katika miaka ya 1980, Dubuis alianzisha karakana yake ya kutengeneza saa huko Geneva. Baada ya kukutana na mfanyabiashara wa Ureno, Carlos Dias, alishawishiwa kuanzisha kampuni ya the Société Genevoise des Montres ambayo baadaye iliitwa Manufacture Roger Dubuis.

Dubuis alistaafu mwaka 2005 ila mwaka 2011 alirudi kwenye kampuni yake kama balozi wake.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Roger Dubuis (mtu) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.