Reli Assets Holding Company
Reli Assets Holding Company (RAHCO) ni shirika la kibiashara lililoundwa na kumilikiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye mwaka 2007. Sheria ya Reli (Railway Act No. 4 of 2002) iliandaa kuundwa kwa shirika[1].
Kazi yake ilikuwa hasa kutunza na kuendeleza miundombinu za reli nchini. Kwa hiyo ilipokea majukumu ambayo hadi wakati ule yalitekelezwa na kumilikiwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC). Sheria ilitaja pia utoaji wa huduma za usafirishaji wa reli lakini iliunda nafasi ya makampuni ambayo yatatekeleza huduma hizo kwa niaba ya RAHCO kwenye njia zinazomilikiwa nayo[2].
Hali halisi huduma hizo zilitekelezwa na Tanzania Railways Limited (TRL), iliyoendeleza sehemu hii ya shughuli ya TRC ya awali ikisimamiwa na kampuni ya RITES kutoka nchini Uhindi.
Kwa hiyo mtandao wa reli ulibaki mikononi mwa serikali ikimilikiwa na RAHCO kama wakala wa serikali.[3]
Huduma za reli na pia hali ya miundombinu zilishuka katika miaka iliyofuata.
Mnamo mwaka 2017 mkataba na RITES ulikwisha. TRL na RAHCO ziliunganishwa tena na TRC ilifufuliwa. Kuanzia hapo huduma zilianza kuboreka tena. TRC ilianzisha pia mfumo mpya wa Reli ya SGR Tanzania inayotumia geji za upana wa milimita 1,435.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ http://repository.businessinsightz.org/bitstream/handle/20.500.12018/322/The%20Railways%20Act%2c%202002.pdf?sequence=1&isAllowed=y Archived 4 Desemba 2021 at the Wayback Machine. The 2002 Railways Act
- ↑ https://www.tanzaniainvest.com/rahco Reli Assets Holding Company (RAHCO), tovuti rasmi
- ↑ Tovuti rasmi