Rasi ya Alaska

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Rasi ya Alaska na volkeno zake
Rasi ya Alaska upande wa kusini ya Alaska Bara

Rasi ya Alaska (kwa Kiingereza: Alaska Peninsula) ni rasi iliyoko kusini magharibi mwa Alaska, kati ya Bahari ya Pasifiki na Bahari ya Bering.

Inaenea kwa umbali wa km 800 kutoka Alaska Bara hadi visiwa vya Aleuti.

Kwa mtazamo tofauti eneo lote la Alaska linaweza kuitwa "rasi" lakini leo hii "rasi ya Alaska" hutumiwa tu kwa ule mkono wa nchi upande wa kusini.

Eneo la rasi ni takriban km 22,000. Idadi ya wakazi ni ndogo, chini ya watu 2,000. Wengi wao ni Maindio na Eskimo.

Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rasi ya Alaska kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.