Nenda kwa yaliyomo

Raqqada

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ukuta wa Raqqada

Raqqāda (kwa Kiarabu: رقّادة) ni kijiji wa Tunisia wenye wakazi 1,000 takriban kilomita kumi kutoka Kairuan. Wakati wa karne ya 9 ulikuwa mji mkuu wa milki ya Waaghlabidi.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 876 Ibrahim II ibn Ahmad, mtawala wa tisa wa Waaghlabidi (875-902), alitaka makazi matulivu nje ya mji Kairuan.

Aliagiza kujengwa kwa majumba ya kifalme pamoja na makazi kwa wakubwa wake, watumishi na wanajeshi, pamoja na msikiti, chuo na soko. Yote yaliviringishwa kwa ukuta mwenye urefu wa kilomita 10.

Aliagiza pia ujenzi wa kiwanda cha karatasi kwa mahitaji ya chuo na wasomi wake. Kuna wakati Raqqada ilikuwa kubwa hata kuliko Kairuan.[1]

Mwaka 909 jeshi la Wafatimiya lilivamia Raqqada na mji ulikuwa mji mkuu wa milki mpya[2] hadi mwaka 969 Wafatimiya walipohamia Kairo nchini Misri. Baada ya uhamisho wa milki Raqqada iliachwa bila wakazi wengi majengo mengi yalibomolewa[3].

  1. (Kifaransa) Musée national d'art islamique de Raqqâda par Mohamed Rebai
  2. Charles Saint-Prot, Islam, l'avenir de la tradition : entre révolution et occidentalisation. Essai, éd. Le Rocher, Paris, 2008, p. 195
  3. Janine et Dominique Sourdel (1 Jan 2004). Dictionnaire historique de l'islam. Paris: French & European Pubns. uk. 702. ISBN 978-0686564461.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Raqqada kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.