Nenda kwa yaliyomo

Raphaël Cishugi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Raphaël Cishugi
Amezaliwa 04 Juni 1967
Walungu, Kivu Kusini
Amekufa Juni 21, 2018 (umri 51)
Bukavu, Kivu Kusini
Nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Majina mengine Jean Raphaël
Kazi yake Mfanyabiashara, mjasiriamali
Miaka ya kazi 1990-2018

Raphaël Cishugi Rugamika (4 Juni 1967 - 21 Juni 2018) alikuwa mfanyabiashara wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mjasiriamali na mshauri. Yeye ndiye mwanzilishi wa Foundation ya GDIBU na aliwahi kuwa mkurugenzi wake mpaka kufa kwake mwaka 2018. Yeye ndiye baba mzazi wa mwandishi wa Kongo Amini Cishugi.[1]

Maisha yake na kazi

[hariri | hariri chanzo]

Raphaël Cishugi Rugamika alizaliwa 4 Juni 1967 huko Walungu (mji wa Kivu Kusini) Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alisoma usimamizi wa biashara shuleni la sekondari na kupata ujuzi wa kuendelea na masomo yake huko Bukavu (mji mkuu wa jimbo) kutoka mzunguko wa nne hadi sita wa sekondari. Alihitimu mwaka wa 1986 katika Shule ya Ubelgiji ya Athens Bukavu. Kazi yake ya kwanza ilifanyika katika kusafirisha sukari ya Kiliba katika eneo la Uvira. Mwanzoni mwa miaka 90, alianza kufanya kazi kama mhasibu katika kampuni ya India Kotesha.

Aliondoka na kuasha kazi katika Kotesha mwaka 2004 baada ya vita vya Kivu. Kisha akafungua duka na kuanza kusafiri kwenda nje ya nchi (Thailand, Dubai, China, India) kununua bidhaa na baada aliwekeza katika ugavi wa maji safi katika wilaya ya Walungu. Katika mwaka 2006, alianzisha GDIBU (msingi wa usaidizi) ambako alikuwa msimamizi mkuu mpaka kifo chake Juni 21, 2018 akiwa na umri wa miaka 51. Mke wake anaitwa Georgine Machozi Nyahengwa na pia yeye alikuwa baba mzazi wa watoto nane.

  1. "Who is Amini Cishugi, the famous author of the story Anna Beckinsales Marie", 243 Stars. Retrieved on 09 Aprili 2019.

Viungo vya njə

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Raphaël Cishugi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.