Nenda kwa yaliyomo

Régis Koundjia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Régis Junior Koundjia-Sindo (alizaliwa Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati, 8 Novemba 1983) ni mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati.[1] Alicheza mpira wa kikapu chuoni LSU Tigers na George Washington Colonials kuanzia 2003 hadi 2007. Koundjia alicheza timu ya taifa ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye Mashindano ya FIBA Afrika mwaka 2005, 2007 na 2009. Alisaini Vermont Frost Heaves inayo shiriki Ligi Kuu (PBL) msimu wa 2008-09 baada ya kucheza Ligi ya Marekani NBA msimu wa joto na San Antonio Spurs.[2]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Baba yake, mwanadiplomasia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, aliuawa kwa kuwekewa sumu mwaka 1991.

Koundjia alisomea sosholojia katika Chuo Kikuu cha George Washington.

  1. https://basketball.eurobasket.com/player/Regis-Koundjia-Sindo/France/ASM-Basket-Le-Puy-en-Velay/89582
  2. https://www.timesargus.com/frost-heaves-sign-cayole-two-others/article_07612f5e-1ff5-5c1e-81ab-bef8ae80306c.html