Nenda kwa yaliyomo

Pweza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pweza
Pweza madoa-meupe
Pweza madoa-meupe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Mollusca (Wanyama bila mifupa wenye ulimi kama tupa)
Ngeli: Cephalopoda
Oda ya juu: Octopodiformes
Oda: Octopoda
Ngazi za chini

Nusuoda 2, familia za juu 2 na familia 12:

Pweza ni wanyama wa bahari wenye minyiri (mikono) minane inayobeba vikombe vya kumung'unyia na inayotumika kwa kukamata wanyama wadogo. Wana domo linalofanana na lile la kasuku ili kuseta gegereka na kome. Spishi nyingi huingiza sumu inayopooza mawino.

Pweza hunaogelea kwa kuondoa maji kwa nguvu kupitia mrija (siphon) wake. Wanaweza kubadilisha rangi yao na pengine umbo wao ili kufanana na kinyume na kujificha kwa mawindo na maadui. Wakivumbuliwa huruka wakitoa ghubari la kiwi (maada kama wino) ili kukanganya adui.

Pweza wanaweza kushambulia watu lakini hii ni adimu. Wakichochewa wanauma kwa domo lao na wanatoa sumu, lakini spishi moja tu, pweza mizingo-buluu, ana sumu inayoweza kuua watu

Kama chakula

[hariri | hariri chanzo]

Kiumbe huyu huliwa sana na watu waishio pembezoni mwa bahari kwa sababu ana nyama nzuri tu, ila huwa na chumvi nyingi.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pweza kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.