Muumakondoo
Muumakondoo | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Muumakondoo madoadoa (Psammophylax rhombeatus)
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 6:
|
Waumakondoo ni nyoka wa jenasi Psammophylax katika familia Lamprophiidae. Wamepewa jina hili kwa sababu watu walifikiri kwamba nyoka hawa wanaweza kuuma kondoo. Lakini hiyo si kweli. Meno yao ni madogo na yapo nyuma katika taya. Isitoshe sumu yao siyo kali sana na haiwezi kuua mnyama mkubwa.
Nyoka hawa sio warefu sana. Muumakondoo milia wa Kenya anaweza kufika m 1.4 lakini kwa kawaida nyoka hawa ni sm 50-90. Kinyume na nyoka wengine madume ni wakubwa kuliko majike. Wana milia ya rangi nyeusi, kijivu, kahawia na/au njano. Milia myeusi inaweza kuwa mbagombago au kugawanyika katika mistari ya madoa.
Waumakondoo hukiakia mchana na hula mijusi na vyura lakini nyoka wengine wadogo na vipanya pia na pengine hata samaki.
Nyoka hawa wana sumu kali kiasi lakini chonge ni nyuma kwa taya. Kwa hivyo hawawezi kuingiza sumu nyingi katika watu. Spishi kadhaa zikikamatwa zinajifanya kama zimekufa.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Psammophylax acutus, Muumakondoo Pua-ndefu (Beaked skaapsteker)
- Psammophylax multisquamis, Muumakondoo Milia wa Kenya (Kenyan striped skaapsteker)
- Psammophylax rhombeatus, Muumakondoo Madoadoa (Spotted skaapsteker)
- Psammophylax togoensis, Muumakondoo wa Togo (Togolese skaapsteker)
- Psammophylax tritaeniatus, Muumakondoo Milia Kusi (Southern striped skaapsteker)
- Psammophylax variabilis, Muumakondoo Tumbo-kijivu (Grey-bellied skaapsteker)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muumakondoo kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |