Principe
Mandhari
Príncipe ni kisiwa cha pili cha nchi ya Sao Tome na Principe, iliyopo katika bahari ya Atlantiki, karibu na Afrika Magharibi. Jina lamaanisha "Mfalme mdogo" au "Mwana wa mfalme" kwa lugha ya Kireno,
Kisiwa kina urefu wa km 16 na upana wa km 6. Milima yake hufikia mita 927 juu ya UB na ni vilele cha safu za volkeno zilizokua kuanzia sakafu ya bahari hadi kufikia usoni pake. Volkeno hizi ni zimwe, si hai tena.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Principe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |