Hajivale
Mandhari
(Elekezwa kutoka Polyboroides)
Hajivale | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 2:
|
Hajivale au kobeamiti ni ndege mbua wa jenasi Polyboroides, jenasi pekee ya nususfamilia Polyboroidinae katika familia ya Accipitridae. Manyoya yana rangi ya majivu na chini yao ni nyeupe yenye milia myembamba kijivu; mkia ni mweusi mwenye baka jeupe moja au mabaka meupe mawili. Wana kiraka cha upara pande zote za macho isipokuwa hajivale wa Amerika.
Ndege hawa hula wanyama na ndege wadogo, nyoka, mijusi, vyura na wadudu, na hajivale wa Afrika na Madagaska hula machikichi pia. Wanaweza kupanda miti na kukamata makinda ya zuwakulu au goregore ndani ya matundu ya hawa kwa miguu mirefu yao. Hulitengeneza tago lao kwa vijititi juu ya mti na jike huyataga mayai 1-3. [onesha uthibitisho]
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Polyboroides radiatus, Hajivale wa Madagaska (Madagascar Harrier Hawk)
- Polyboroides typus, Hajivale wa Afrika (African Harrier Hawk)
- Polyboroides t. pectoralis, Hajivale Magharibi (Western Harrier Hawk)
- Polyboroides t. typus, Hajivale Mashariki (Eastern Harrier Hawk)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Hajivale wa Madagaska
-
Hajivale wa Afrika