Nenda kwa yaliyomo

PW Botha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Pieter Willem Botha)
P.W. Botha

Pieter Willem Botha (12 Januari 1916 - 31 Oktoba 2006) alikuwa waziri mkuu na rais nchini Afrika Kusini.

Alijulikana kwa majina ya "P.W." na "Die Groot Krokodil" (Afrikaans: "mamba mkuu").

Botha alikuwa mwanasiasa wa asili ya makaburu na waziri mkuu wa Afrika Kusini kati ya 1978 na 1984.

Alikuwa rais wa nchi wa pili kabla wa mwisho katika mfumo wa "apartheid" (ubaguzi wa rangi) kati ya 1984 na 1989.

Botha alifuata siasa ya ubaguzi wa rangi. Alisimamia ujenzi wa bomu ya nyuklia ya Afrika Kusini na upanuzi wa jeshi la taifa.

Katika siasa ya ndani alikuwa na msimamo wa kulipunguza kidogo ukali wa ubaguzi warangi. Alifuta sheria zilizopiga marufuku ndoa kati ya watu wa rangi mbalimbali akaruhusu vyama vya kisiasa vya watu wa rangi mbalimbali. Alipunguza pia ukali wa "Group Areas Act" iliyokataza watu wa rangi fulani kuishi katika eneo la rangi tofauti.

Lakini aliendelea kutazama ANC kama kikndi cha kigaidi akikataa kushauriana na viongozi kama Nelson Mandela. Aliendesha vita za Afrika Kusini katika Msumbiji na Angola.

1989 alilazimishwa kujiuzulu baada ya kupata matatizo ya kiafya. Mfuasi wake alikuwa Frederik W. de Klerk aliyeruhusu baadaye uchaguzi huru wa kwanza nchini na mwisho wa Ubaguzi wa rangi.