Nenda kwa yaliyomo

Ukukwi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Philothamnus)
Ukukwi
Naranyasi au ukukwi mabaka (Philothamnus semivariegatus)
Naranyasi au ukukwi mabaka (Philothamnus semivariegatus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Colubridae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri)
Oppel, 1811
Nusufamilia: Colubrinae
Jenasi: Philothamnus
Smith, 1840
Ngazi za chini

Spishi 20:

Kukwi ni spishi za nyoka kijani wa jenasi Philothamnus katika familia Colubridae wasio na sumu. Spishi nyingine huitwa isale, namalanga, naranyasi, ngowe au nyokameni.

Kwa kawaida urefu wa nyoka hawa ni chini ya m 1, mara nyingi sm 50-100 na hadi 130 kwa kipeo. Rangi yao ni kijani pengine pamoja na rangi nyingine kame kijivu, buluu, nyekundu na njano. Spishi kadhaa zina madoa. Nyokameni ni mwekundu au kahawianyekundu.

Nyoka hawa wanatokea karibu na maji mara nyingi kwa sababu takriban spishi zote hula vyura na ndubwi zao. Lakini hupita masaa mengi mitini ambapo huwinda mijusi na vyura-miti.

Kukwi hawana sumu lakini wanaweza kung'ata na wakifanya hii husogea kichwa huku na huku ili kusababisha mikwaruzo mibaya.

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukukwi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.