Nenda kwa yaliyomo

Peter K. Palangyo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Peter K. Palangyo (1939 - 18 Januari 1993) alikua mwandishi wa riwaya na mwanadiplomasia.

Sifa yake iliangukia kwenye riwaya yake ya Dying in the Sun (1968), ambayo inachukuliwa na wengi kama moja ya kazi nzuri za kisasa kwenye uandishi wa Kiafrika.[1]

Mzaliwa wa Arusha, Palangyo alisomea huko, pia alisoma Uganda na Marekani. Alisomea biolojia katika chuo cha St. Olaf College huko Northfield, Minnesota, pia alienda shule ya kuhitimu kule University of Minnesota.

Aliachana na sayansi kwa ajili ya fasihi, akaenda kuchukua stashahada ya ualimu kutoka Chuo Kikuu cha Makerere na alifundisha shule kadhaa za sekondari. Mnamo mwaka 1968 alirudi Marekani na kujiunga na waandishi wa University of Iowa, na akapata MFA kwenye uandishi bunifu. Alirudi Tanzania mwaka 1972, akafundisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla ya kujiunga na huduma ya kidiplomasia. Wakati mmoja aliweza kuwa Balozi wa Tanzania huko Ufaransa. "[1] Mwaka 1980 alipata PhD kutoka University at Buffalo, The State University of New York, na nadharia kwenye Chinua Achebe.[2]

Palangyo alifariki mwaka 1993 kwenye ajali ya gari."[1]

  1. 1.0 1.1 1.2 Simon Gikandi (2007). "Palangyo, Peter K. (1939-1993)". Katika Evan Mwangi, Simon Gikandi (mhr.). The Columbia Guide to East African Literature in English Since 1945. Columbia University Press. ku. 136–7. ISBN 978-0-231-12520-8. Iliwekwa mnamo 19 Novemba 2012.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Palangyo, The African sense of self with special reference to Chinua Achebe : a dissertation, PhD thesis, State University of New York at Buffalo, 1980.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Peter K. Palangyo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.