Nenda kwa yaliyomo

Penina Muhando

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Penina Muhando
Amezaliwa 1948
Morogoro
Nchi Tanzania
Kazi yake Profesa

Penina Muhando, pia anajulikana kama Penina Mlama alizaliwa 1948, ni mnadharia na pia ni mwandishi wa tamthilia za Kiswahili kutoka nchini Tanzania.

Maisha na kazi yake

[hariri | hariri chanzo]

Muhando alizaliwa Berega Mkoa wa Morogoro nchini Tanzania mwaka 1948. Alipata shahada ya sanaa,shahada ya elimu,na pia shahada ya uzamivu kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Alifanikiwa kuwa profesa na pia kiongozi wa idara ya sanaa ya maigizo katika chuo kuu cha Dar es Salam.[1][2]

Muhando alikuwa mmoja kati ya kundi la waandishi wa sanaa za maigizo Tanzania katika kipindi cha mwishoni mwa mwaka 1960, na mwanzoni mwa mwaka wa 1970, walioibuka baada ya azimio la Arusha chini ya rais Julius Nyerere mwaka 1967. Ujamaa ilikuwa ni falsafa ya nchi. Katika mazingira haya sanaa ya maigizo haikuwa ikiungwa mkono na wengi. Waandishi wengi walikuwa wakiitwa na Nyerere kutumia sanaa yao kama njia ya kuutangaza ujamaa kwa watu wa Tanzania na pia kutumia sanaa kama njia ya kujiletea maendeleo.[3]

Muhando alikutana na changamoto katika uandishi baina ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kwa kutumia lugha ya Kiingereza kungepelekea kufungua zaidi soko la nje lakini pia isingeleta tija kwani idadi kubwa ya watanzania hawatumiii lugha ya kiingereza. Lakini pia lugha ya kiswahili ingewezesha idadi kubwa ya watanzania kufuatitlia lakini pia ingepoteza soko la nje. Licha ya hayo Muhando alilamua kuandika katika lugha ya kiswahili kwa sababu aliona yakuwa maigizo kama ni silaha muhimu ya kufikisha ujumbe kwenye jamii na pia ni lugha inayotumika na wazawa wengi na hilo ndilo lilikuwa la msingi.

Baadhi ya vitabu vyake

[hariri | hariri chanzo]
  1. Ada U. Azodo, "Muhando, Penina", in Jane Eldredge Miller (ed.), Who's Who in Contemporary Women's Writing, Routledge, 2001, pp. 226–227.
  2. Griffiths, Gareth (2014). id=S2GPBAAAQBAJ African Literatures in English: East and West. Routledge. uk. 381. {{cite book}}: Check |url= value (help); Missing pipe in: |url= (help)
  3. Chambers, Colin, mhr. (2002). "Tanzania". The Continuum Companion to Twentieth Century Theatre. Continuum. ku. 746–747.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Penina Muhando kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.