Orodha ya wapiga gitaa wa Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Hii ni orodha ya wapiga gitaa maarufu barani Afrika.

Kialfabeti[hariri | hariri chanzo]

 • Barthelemy Attisso - mpigaji gitaa kiongozi wa bendi ya Orchestre Baobab, huko nchini Senegal.
 • Omara "Bombino" Moctar - mpigaji maarufu, mwimbaji na mtunzi kutoka mjini Agadez, Niger.
 • Alick Macheso - mpigaji gitaa mkuu wa bendi ya Orchestra Mberikwazvo, nchini  Zimbabwe.
 • Oliver De Coque - wa Ogene Sound Super of Africa
 • Mamadou Diop (pia anajulikana kama Modou Diop) - mpiga rizim gitaa wa kutoka Senegal, lakini kwa sasa yupo nchini Marekani
 • Afel Bocoum - Mpiga gitaa marufu kutoka nchini Mali, Ali Farka Touré ndiye mwalimu wake
 • Henri Bowane - Ni mtu mkubwa katika masuala mazima ya uanzishwaji wa rumba la Kikongo, wanafunzi wa awali wa Franco.
 • Diblo Dibala -  Mwanamuziki wa Kikongo ambaye maarufu kwa mtindo wa soukous, anafahamika kama "Machine Gun" kwa kasi na maarifa yke ya juu katika upigaji mzima wa gitaa.
 • Nico Kasanda (aka "Dr. Nico") - mmoja kati ya waanzilishi wa muziki wa soukous.
 • François Luambo Makiadi (aka "Franco") - Mwanamuziki wa Kikongo, mwanzilishi wa kundi zima la muziki wa Jazz maarufu OK Jazz.
 • Nico Mbarga - mpigaji gitaa mkuu na mtunzi maarufu wa wimbo maarufu wa "Sweet Mother."
 • Oliver Mtukudzi - Mpigaji gitaa kutoka nchini Zimbabwe na kiongozi wa 'Black Spirits'
 • Jean-Bosco Mwenda - Mwanzilishi wa mtindo wa Kiafrika maarufu "mtindo wa kidole" katika miaka ya 1950, Kongo
 • Ray Phiri- Mpigaji gitaa marufu kutoka mjini Mpumalanga, Afrika Kusini
 • Jonah Sithole Mpigaji gitaa kutoka nchini Zimbabwe, anapiga na Thomas Mapfumo
 • Djelimady Tounkara, mpiga gitaa maarufu wa bendi ya Super Rail Band kutoka mjini Bamako, Mali.
 • Ali Farka Touré - mwimbaji na mpiga gitaa kutoka nchini Mali.
 • Vieux Farka Touré - mtoto wa Ali Farka Touré, anachipukia kutoka nchini Mali.
 • Sir Victor Uwaifo- Mpigaji gitaa kutoka kwa watu wanaongea Kibini/Kiedo, yupo mjini Benin, Jimbo la  Edo, Nigeria.
 • Dr Sir Warrior - Mwimbaji na Mpigaji gitaa wa bendi ya Oriental Brothers International Band
 • Jonah Sithole - Mpiga mbira na gitaa marehemu ambaye awali alikuwa anapiga na Thomas Mapfumo
 • Joshua Dube - Mpigaji gitaa hayati ambaye awali alikuwa akipiga na Thomas Mapfumo
 • Habib Koité - mwimbaji na mpigaji gitaa kutoka nchini Senegal