Orchestra Baobab

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Orchestra Baobab wakitumbuiza Brooklyn Juni 2008

Orchestra Baobab ni bendi maarufu ya muziki wa dansi toka nchini Senegal. Bendi hii imekuwepo katika ramani ya muziki wa Afrika toka ilipoanzishwa mwaka 1970.

Orchestra Baobab inapiga muziki ambao ni mchanganyiko wa vionjo vya muziki toka Cuba, Visiwa vya Karibiani na Afrika. Baada ya kupata mafanikio makubwa na kuweza kurekodi albamu 20 toka mwaka 1970 hadi 1985, bendi hii ilivunjika mwaka 1987. Hata hivyo mwaka 2001 Orchestra Baobab iliibuka upya na kurekodi vibao vyao vya zamani na kufanya ziara katika nchi kadhaa za Ulaya. Pamoja na kutoa vibao vyao vya zamani, walirekodi nyimbo mpya wakisindikizwa na mwanamuziki maarufu wa Senegal, Youssou N'dour na Ibrahim Ferrer, mwanamuziki maarufu toka Cuba.

Mwaka 2003 Orchestra Baobab ilipata nafasi ya kuweko kwenye filamu iliyotengenezwa na wanamuziki Dave Matthews na Trey Anastasio iitwayo Trey and Dave Go to Africa. Katika filamu hiyo wanamuziki hao walifanya onyesho pamoja na Orchestra Baobab.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]